info@healingmissionaries.or.tz Dar es Salaam, Tanzania
Bringing hope, healing and transformation through worship, ministry and community outreach
Dedicated to serving God and transforming lives through worship, ministry, discipleship and community outreach.
Mimi ni mjasiriamali ninayejishughulisha na biashara mbalimbali, kwa lengo la kutengeneza thamani, kuleta maendeleo, na kutoa suluhisho katika jamii kupitia shughuli zangu za kibiashara. Mimi ni mtumishi wa Mungu kupitia huduma ya uimbaji. Ninaamini kuwa muziki ni njia ya kuhubiri Injili, kuleta faraja, matumaini, na kuwavuta watu karibu zaidi na Mungu. Zaidi ya yote, ninapenda sana kuwasaidia watu. Furaha yangu kubwa ni kuona maisha ya mtu yanabadilika kwa sababu nimeweza kumsaidia kuvuka changamoto aliyokuwa anakabiliana nayo. Kuona mtu akifanikiwa au akipata tumaini kupitia mchango wangu ni jambo linalonipa moyo na kunifanya niendelee kutenda mema. Vilevile, ninathamini sana muda ninaoutumia na familia yangu. Kwangu, familia ni nguzo ya upendo, amani, na nguvu, na ndiyo sehemu ninayopata faraja, hamasa, na msukumo wa kuendelea kutimiza ndoto zangu.
Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 1 Yohana 5:!4